Jeremiah 46:13-26

13 aHuu ndio ujumbe Bwana aliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:

14 b“Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,
hubiri pia katika Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
na Tahpanhesi:
Ni mji katika Misri.

‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,
kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’
15 eKwa nini mashujaa wako wamesombwa
na kupelekwa mbali?
Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana
atawasukuma awaangushe chini.
16 fWatajikwaa mara kwa mara,
wataangukiana wao kwa wao.
Watasema, ‘Amka, turudi
kwa watu wetu na nchi yetu,
mbali na upanga wa mtesi.’
17 gHuko watatangaza,
‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,
amekosa wasaa wake.’

18 h“Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,
ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,
“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,
kama Karmeli kando ya bahari.
19 iFunga mizigo yako kwenda uhamishoni,
wewe ukaaye Misri,
kwa kuwa Memfisi utaangamizwa
na kuwa magofu pasipo mkazi.

20 j“Misri ni mtamba mzuri,
lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.
21 kAskari wake waliokodiwa katika safu zake
wako kama ndama walionenepeshwa.
Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,
hawataweza kuhimili vita,
kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,
wakati wao wa kuadhibiwa.
22 lMisri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia
kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,
watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,
kama watu wakatao miti.
23 mWataufyeka msitu wake,”
asema Bwana,
“hata kama umesongamana kiasi gani.
Ni wengi kuliko nzige,
hawawezi kuhesabika.
24 nBinti wa Misri ataaibishwa,
atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”
25 o Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,
Thebesi kwa Kiebrania ni No (au No-Amoni), mji katika Misri.
na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.
26 qNitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asema Bwana.

Copyright information for SwhNEN